WASIMAMIZI WA MIRADI YA TASAF KUHAKIKISHA WANASIMAMIA KIKAMILIFU

 

Wasimamizi wa miradi ya tasaf wametakiwa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi hiyo kuhakikisha kuwa changamoto zilizojitokeza katika miradi iliyipta hazijirejei tena.

Katibu mkuu afisi ya makamu wa pili wa rais dk. Idris muslim hija amesema lengo la miradi hiyo ni kuona kuwa kaya zilizo kwenye mpango wa ajira za muda zinaufaika kupitia miradi iliyobuliwa.

Dk. Idris alikuwa akizungumza na watoa huduma ngazi za jamii katika utekelezaji wa miiradi ya kutoa ajira za muda ambapo amesema kulikuwa na changamoto kadhaa ambazo zinaweza kusababisha mradi kutofikia malengo hivyo amewataka kila mmoja kutimiza jukumu lake.

Kwa upende wake mkurugenzi iuratibu shughuli za smz khalid bakari hamrani amesema kwa vile zanzibar ni moja ya eneo linalofanya vizuri katika utekelezaji wa miradi ya tasaf hivyo ni vyema wasimamizi wa miradi hiyo kupita kwa walengwa ili miradi iwe endelevu.