WASIMAMIZI WA MITIHNI YA TAIFA YA KIDATU CHA NNE WA WAMETAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA USIMAMIZI

 

 

Wasimamizi wa mitihni ya taifa  ya kidatu cha nne wa wametakiwa kufuata taratibu za usimamizi wa mitihani  na kujiepusha na udanganyifu ili kuanikisha mitihani hiyo kufanyika kwa amani.

Akizungumza na walimu wanaotarajiwa kusimamia mitihani ya kidato cha nne skuli za mkoa wa kusini katibu tawala wa mkoa huo bi fatma moh’d juma amesema  uzoefu wao isiwe ni chanzo cha kuepuka taratibu za mitihani nakuwataka kufanya kazi zao  kwa ufanisi ili wanafunzi waweze kufanya mitihani yao kwa ufanisi.

Nae mkuu wa polisi mkoa wa kusini suleiman hassan suleiman amesema jukumu la askari katika vituo vya mitihani ni kukilinda usalama wa maeneo hayo ili kuepuka uvujaji wa mitihani na kuhakikisha kuwa mitihani inafanyika kwa salama na amani.