WASIMAMIZI WA UJENZI WA BARABARA KUZINGATIA MIONGO YA MVUA

 

 

Wasimamizi wa ujenzi wa barabara  wametakiwa kuzingatia miongo ya mvua  ili kuepusha  hasara  kama  ilivyo jitokeza  katika  baadhi  ya  barabara  zilizo anza  kufanyiwa  matengenezo.

Miongoni   mwa barabara  zilizoanza  kufanyiwa matengenezo kwa hatua  ya kwanza  na kuharibiwa vibaya  na  mvua  zinazo endelea kunyesha  ni  michenzani ambayo imekuwa ikilalamikiwa  kwa kusababisha usumbufu kwa vyombo  vya usafiri.

Akizungumza  wakati  wajumbe wa bodi  ya mfuko wa barabara  walipokagua barabara mbalimbali , mkurugenzi  mkuu wa mfuko wa barabara nd mwalim ali mwalim amesema  wahandisi  wa ujenzi  ni vyema  wakazingatia  mwenendo  wa hali ya hewa ili  kuepusha  hasara kama ilvyo jitokeza katika  barabara  hiyo  ambayo ilikuwa  imebakisha hatua ya kuwekewalami.

Amesema jitihada  zina fanyika  kuhakikisha  barabara hiyo  inafanyiwa matengenezo  kwa kipindi  kifupi kijacho na kuwaomba wananchi  kuwa wastahamilivu .

Barabara  nyengine zilizo kaguliwa ni saateni shauri moyo, kwarara, kwa mabata  kijitoupele, kilombero mgonjoni,  kinduni kichungwani, na barabara ya  kifusi ya donge  muwanda inayoendelea  na ujenzi wa mtaro, ambapo  mhandisi  kutoka  idara ya  ujenzi na utunzaji  wa  barabara japhet malambi amesema ujenzi huo ni kwa ajili  ya kulinda barabara  hiyo isiharibike na mvua.