WATAALAMU WA MASUALA YA URITHI WA UTAMADUNI WAMESEMA KUNA UPUNGUFU MKUBWA

Wataalamu wa masuala ya Urithi wa Utamaduni  kutoka nchi za Afrika ya Mashariki, wamesema kuna upungufu Mkubwa wa uhifadhi hasa katika usimamizi wa shughuli hizo.

wamefahamisha mbali na mapungufu hayo pia majanga ya kimaumbile na yanayosababishwa na binaadamu yanachangia kupunguza ustawi wa maeneo mengi ya kihistoria katika nchi husika.

wakiwasilisha mada katika mkutano wa kimataifa kuhusu urithi wa utamaduni kwa nchi za afrika ya mashariki wamesema kuwa simamizidhaifu na ukosefu wa utafiti katika majenzi mbalimbali ndio chanzo kikuu cha uharibifu wa maeneo hayo.

wamesema nchi za Afrika ya mashariki zina raslimali nyingi za Urithi wa utaaduni ambazo zinahitaji taaluma ya kuzitunza ili ziweze kuleta tija kwa mataifa yao na watu wake.

hata hivyo mkutano huo wa siku tatu umeazimia kuweka mikakati ya pamoja kuona udhibiti wa urithi wa utamaduni unaimarika kwa kushirikiana kikamilifu na Serikali za nchi husika.

mkutano huo ambao umefanyika Zanzibar, umeshirikisha wataalamu mbalimbali, nchi zilizoshiriki ni pamoja na tanzania bara, Kenya, Uganda, Rwanda, Comoro, Mauritius, Msumbiji na mwenyeji wake Zanzibar.