WATAFITI NCHINI WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZILIZOPO ZA UCHUKUAJI WA VIBALI KWA AJILI YA KUFANYA UTAFITI

Mtakwimu mkuu wa serikali ya mapinduzi zanzibar bi mayasa mahfoudh amesema ni wajibu wa watafiti nchini kufuata sheria na taratibu zilizopo za uchukuaji wa vibali kwa ajili ya kufanya utafiti wa masuala mbali mbali.
Bi mayasa mahfoudh mwinyi amebainisha hayo wakati akijibu maswali kwa washiriki wa mafunzo ya matumizi ya takwimu na kusema ni vyema serikali kutambua tafiti zote zinazofanyika nchini ili kupata taarifa zake kwa.
Amesema hatua hiyo itasaidia udhibiti wa utoaji wa takwimu kiholela zinazochangia kuleta mgongano wa kitakwimu kwa jamii.
Wakitowa michango yao washiriki wa mafunzo hayo wamesisitiza kutumika vyema kwa sheria iliyopo ili kuwawezesha wazalishaji wa taarifa kutambua umuhimu wao katika mipango ya maendeleo ya nchi.