WATAKIWA KUJUA HAKI ZAO KATIKA USAFIRI

 

Wanachi wametakiwa kujua haki zao pale wanapopata huduma za usafiri ili kuondosha malalamiko kwa madereva na makonda

Mkuu wa mkoa mjini magharib  mhe ayoub mohd mahamoud akizindua kampeni ya abiria paza sauti wakiwa katika gari za abiria ili kuwaokoa na kadhia mbali mbali kwa madereva na matingo wakorofi wakiwa katika safari zao .

Amesema kumekuweko na malalamiko ya chini kwa chini kwa wanachi wakizilalamikia kero za baadhi ya madereva bila ya kujua kero hizo  wananchi wayafikishe wapi hivyo kupitia kampeni hiyo ambayo imeenda sambamba na utowaji wa namba ya simu itakayomrahisishia mwananchi kupiga simu kwa askari wa usalama barabarani

Aidha   mahamoud  akizitaja kero hizo ni mwendo wa kasi kupelewa abiria kutokufikishwa ktk vituo wanavyoshukia  lugha chafu kwa makonda na kupandishiwa nauli .

Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi ambaye pia ni mkuu wa kikosi chausalama barabarani mkadam khamis mkadamamesema lengo la kampeni hiyo ni kupunguza ajali barabarani ambazo zimekuwa nyingi zinazosababishwa na madereva wazembe.

Kwa upande wa wanachi wamekuwa na haya ya kusema kuhusiana na kampeni hiyo ambapo katibuwamtandaowa mabalozi wa usalama barabarani  amesema zoezi hilo litafika hadi pema kwa kuwapa wnchi elimu .

Wakati huo huo  mhe ayoub ameshiriki  katuika matembezi ya baraza la vijana ikiwa maadhimisho ya kuitmiza mwaka mmoja wa baraza la vijana wilaya ya mjini  tangu kuanza kwake liloendelea na uchangiaji wa damu.