WATEJA WANAOTUMIA BENKI YA FBME WAMELALAMIKIA UWAMUZI ULIOCHUKULIWA NA BENK

 

Wateja  wanaotumia benki ya fbme wamelalamikia  uwamuzi uliochukuliwa na benk  hiyo  wa kutaka  kuwalipa kiasi kidogo cha fedha kinyume na madeni wanayodai baada ya benki hiyo kufungwa kwa zaidi ya miezi sita sasa.

Wateja hao ambao walikuwepo eneo la benki hiyo wamesema wameshtushwa na tangazo lililobandikwa katika eneo la benki linaloelezea ukomo wa malipo ya fidia kwa mujibu wa sheria ya benki na taasisi za fedha mwaka 2006 kuwa fidia ya bima ya amana si zaidi ya shilingi milioni moja na laki tano.

Wamesema tangazo hilo limewashtusha kwa vile hawajui ni muda gani watamaliziwa fedha zao wanazodai licha ya kuwa baadhi yao wana kiwango kikubwa cha fedha walizoweka akiba katika  benki hiyo.

Wanchi hao  walifika katika  benki  hio tokea  saa  mbili  za asubuhi  hadi  saa sita  mchana ndipo walipoanza kupatiwa  huduma za  usaili kwa ajili ya maandalizi  ya  kupatiwa fedha zao siku inayofuata.

Hata hivyo  uongozi wa benki hiyo  haukua tayari kuzungumza na vyombo  vya habari  kwa madai  ya kutingwa  na kazi ya  kuhudumia  wateja.

Benk ya fbme  ilifutiwa leseni ya  kufanya  shughuli za kibenki na benki kuu ya tanzania  bot  mnamo tarehe 8 mwezi mei 2017 ambapo bodi ya bima ya amana ikatangaza  kuanza kulipa fidia ya kuanzia tarehe  01 nov 2017.