WATENDAJI KUACHA TABIA YA KUWA NA MASLAHI BINAFSI

 

Waziri wa fedha na mingango dr halid slum mohammed amewataka baadhi ya watendaji kuacha tabia ya kuwa na maslahi  binabsi katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

amesema hivi sasa kuna baadhi yao wanaonekana kutofuata taratibu za kazi katika kuwatumikia wananchi

dr khalid amesema hayo wakati akizungumza na watendaji wa mfuko wa hifadhi ya jamii zsssf katika kikao cha utekelezaji wa mpango na mkakati pamoja na kutatua changamoto za utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2018 -2019 kilicho fanyika ndani ya ofisi za zssf kilimani.

Amesema kila mtendaji   anahaki ya kufanya kazi kwa uwadilifu, ubunifu na kuibua mapungufu na kasoro zilizopo  kwa lengo la kutekeleza  yale ambayo anayoyasimamia.

hata hivyo  amesema zsssf ndio chombo muhimu kwa maslahi  ya nchi na wananchi hivyo kila mtendaji  hana budi kutekeledha dhima aliyopewa.

Mapema dr khali ametembelea jengo la treni darajani na  kupata maelezo  , kuangalia eneo litakalo jengwa shoping mol michenzani na kuangalia nyumba za kisasa mbweni .

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo  dr khalid amesema serikali  haitosita kumchukulia hatua mkandarasi yoyote atakae kiuka mashariti yaliopangwa na kuwataka wakandarasi hao kumaliza kwa wakati  nyumba hizo ambazo zimegharimu  shilingi bilioni 43 nukta 7.

Imepanga mipango madhubuti kwa wananchi wake  hivyo amewataka wajenzi wa majengo hayo kumaliza kwa wakati zinazojengwa na mfukowa hifadhi ya jamii