WATENDAJI KUFANYAKAZI KWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA

 

 

 

katibu tawala mkoa wa kusini bi: fatma muhammed juma amewataka watendaji wa halmashauri ya wilaya ya kaskazini b kufanyakazi kwa kufuata sheria na kanuni za utumishi wa umma ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.ameyasema hayo huko kinduni wakati  akizungumza na watendaji wa halmashauri hiyo, chama na  kamati ya ulinzi na usalama ya wilya ya kaskazini ‘b’amesema serikali inawajali watendaji wake lakini haitasita kuwachukulia hatua endapo wataekwenda kinyume na sheria za utumishi na  kutotimiza wajibu wao.

mkuu wa wilaya ya mkoani pemba ambae alikuwa mkuu wa wilaya ya kaskazini b bw: issa juma ali amewaomba viongozi wapya walioteuliwa hivi karibuni kufanyakazi kwa kushirikiana ili kuiletea maendelea wilaya hiyo.kwa upande wake katibu tawala wilaya ya kaskazini b bw: makame machano haji amewaomba viongozi wa chama na serikali na kamati ya ulinzi na usalama kumpa mashirikiano na kuahidi kuyaendeleza yaliyoachwa na viongozi waliopita .