WATENDAJI WA BARAZA LA MANISPAA KUFANYA KAZI WALIZOPANGIWA

 

Watendaji wa baraza la manispaa magharibi b wametakiwa kufanya kazi kama waliopangiwa ili kufikia lengo la serikali kupitia sekta ya ugatuzi.

Hayo yameelezwa na naibun waziri ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa na vikosi maalum vya sms mh. Shamata shaame khamis wakati akizungumza na watendaji hao huko ofisi ya manispaa magharibi ‘b’  kwamchina mwisho.

Amesema suala la ugatuzi ni jambo la kisheria na ni maamuzi ya serikali na hivyo hakuna mtumishi  yoyote atakaepingana na maamuzi hayo ambayo yamekwisha kupitishwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar.

Hata hivyo amesema lengo kuu la kikao hicho ni kuwakumbusha watendaji wa sekta mbali mbali wa manispaa hiyo ili ukusanyaji wa mapato uweze kuongezeka na kuwataka wafanyakazi hao kujenga mashirikiano.

Mkurugenzi wa baraza la manispaa magharibi ‘b’  amour ali mussa  amesema kupitia suala la masoko tayari chombo hicho kimemtafuta injinia wa ujezi soko hilo ili wafanya biashara wazeweze kuuza biashara zao.

Nao baadhi ya watendaji hao wamemshukuru naibu waziri huyo kwa ujio wake na kuwaomba wafanyakazi wezao kufanya kazi kwa kufuata sheria na misingi ya katiba  ili kuweza kuongeza mapato kwa mwaka wa mpya wa fedha  na kufikia malengo ya serikali.