WATENDAJI WA SHIRIKA LA BANDARI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

Naibu waziri wa ujenzi mawasiliano na usafiri shaji mh mohamed ahmada salum amewataka watendaji wa shirika la bandari kufanya kazi kwa uadilifu ili kwenda sambamba na kasi ya ushindani kibiashara.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa upakizi na upakuaji makontena ya mizigo bandarini malindi amesema zanzibar imekuwa inategemea mapato kutokana na bandari ambapo asilimia tisini ya mizigo hupitia bandarini.
Ameongeza kuwa ni jukumu la wafanyakazi wa sekta hiyo kuhakikisha wanajiepusha na suala la vitendo vya uhujumu uchumi ikiwemo kupokea rushwa.
Nao baadhi ya wafanyaki wa shirika la bandari kitengo cha mizigo wamesema wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na taasisi zote za udhibiti wa mapato na kuahidi kuondosha changamoto zote zinazojitokeza.
Wakati huo huo mhe ahmada alitembelea karakana ya gari chumbuni na kukagua ujenzi wa barabara ya kizimbani miwani yenye urefu wa kilomita 7 nukta 2 na kuahidi ujenzi huo kukamilika kama ilivyopangwa.