WATENDAJI WA YA MUFTI KUTEKELEZA KAZI KWA UADILIFU WANAPOTOA TALAKA

 

 

 

Waziri wa nchi ofisi ya rais katiba, sheria, utumishi wa umma na utawala bora mhe. Haroun ali suleiman amewataka watendaji wa ofisi ya mufti na kamisheni ya wakfu na mali ya amana kutekeleza kazi kwa uadilifu wanapotoa maamuzi ya mirathi na talaka.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wafanyakazi wa ofisi ya kamisheni ya wakfu na mali ya amana pamoja na watendaji  wa ofisi ya mufti kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya rais katiba sheria utumishi wa umma na utawala bora uliiopo mazizini, wilaya ya magharibi b.

Mwalimu haroun amewataka watendaji wa ofisi hizo kuhakikisha wanaepukana na vishawishi vinavyopelekea kutoa maamuzi yasiyo sahihi.Amesema faida kubwa ya uadilifu  inatapatikana kwa mwenyezi mungu.

Mapema wawakilishi wa ofisi ya mufti na kamisheni ya wakfu na mali ya amana walitoa taarifa za hatua zinazoonyesha mafanikio katika taasisi zao.

Mufti mkuu wa zanzbar sheikh  saleh omar kabhi amesisitiza umuhimu wa amani na upe4ndo pamoja na umuhimu wa kupatiwa elimu wafanyakazi wa taasisi hizo.