WATOA HUDUMA KATIKA TAASISI ZA SERIKALI NA BINAFSI KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

Naibu waziri wizara ya kazi, uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto, shadya mohamed suleiman amewataka watoa huduma katika taasisi za serikali na binafsi kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake wazingatie sheria katika utendaji wao wa kazi, ili kutokomeza vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwenye maeneo ya kazi na jamii kwa ujumla.

Mh: shadya  ametoa kauli hiyo  alipokuwa akifungua mkutano wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wahanga wa majumbani na sehemu za kazi kwa waathiriwa wa vitendo vya ukatili na udhalilishaji, ikiwa ni katika maadhimisho ya  siku 16 za kupinga ukatili na  udhalilishaji, uliofanyika katika Ukumbi wa baraza la Mji Chake Chake.

Amesema , vitendo vya udhalilishaji katika sehemu za kazi vipo, jambo ambalo linapelekea kukosekana kwa utendaji kazi ulio bora, ambao hudumaza maendeleo na kuwataka watoa huduma kufanya kazi kwa kuisaidia jamii, ili kutokomeza vitendo hivyo.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar, Nasma Haji Choum amesema, lengo la kuadhimisha siku hiyo ni kumaliza matendo ya  udhalilishaji, ambapo ujumbe wa mwaka huu ni ‘Tulinde nguvu kazi tumalize vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia katika sehemu za kazi’.

Kwa upande wake Mratibu wa dawati la wanawake  Mkoa wa kaskazini  Fakihi Yussuf  aewataka wahanga wa vitendo vya udhalilishaji kuwa na usiri wakati vyombo vya sheria vinapofuatilia  kesi zao ili kutokuwapa mwanya watuhumiwa kukimbia.

 

 

 

No Comments Yet.

Leave a comment

Powered by Live Score & Live Score App