WATOTO 105 WAMEREJESHWA MASKULINI BAADA YA KUTOROKA

 

 

 

Jumla ya watoto 105 wamerejeshwa maskulini baada ya kutoroka na 10 wamerejeshwa baada ya kufanyiwa vitendo vya kudhalilishaji katika mkoa wa kaskazini unguja.

Wakitoa maelezo juu ya mpango kazi katibu wa  jumuiya wanawake na maendeleo hidaya ali katibu wa  jumuiya ya kupambana na udhalilishaji  ali makame  wamesema bado jamii inahitaji kupewa elimu juu ya vitendo vya udhalilishaji pamoja na umuhimu wa elimu hasa kwa mtoto wa kike.

Wamesema mbali na hayo pia kumekuwa na matatizo  mbali mbali yanayochangia watoto wa kike kusoma katika mazingira mabaya yakiwemo masuala ya vyoo.

Wakitoa ushuhuda wao baadhi ya wanafunzi waliorejeshwa maskulini wamesema sababu kuu ya kutoroka ni kutokana na maisha magumu yanayozikabili familia zao pamoja na ukosefu wa vifaa vya kusomea.

Wamese pamoja na kuendelea na masomo lakini wameomba wafadhili mbali mbali kuwasaidia ili waweze kuendelea na masomo yao kwa urahisi

Jumuiya hizo zinafanya kazi kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari wanawake tamwa kupitia miradi ya utetezi na kuwainua wanawake kiuchumi  chini ya ufadhili wa foundation for civil society na ubalozi wa  canada