WATOTO 14 WAMEZALIWA KATIKA USIKU WA MKESHA WA KUAMKIA IDDIL HAJJI

 

Jumla  ya  watoto 14  wamezaliwa  katika   usiku  wa  mkesha  wa  kuamkia  iddil  hajji  katika  hospitali  kuu  ya  mnazimmoja

Akitoa  taarifa  ya  wa  kuzaliwa  kwa  watoto  hao  muuguzi  wa  zamu  zainab  hassan  suleiman  amebainisha  kuwa katika  idadi  hiyo  wanane  ni  wanawake  na  6  ni  wanaume wakati hadi  sasa  hali  zao  zinaendelea vizuri. Jumla  ya  wazazi  13   wamejifungua  kwa  njia  ya  kawaida  na  mmja  kwa  upasuaji.

Amesema  jumla  ya  wazazi   13  wamejifungua  kwa  njia  ya  kawaida    na mmoja  kwa  upasuaji  ambapo  kati  ya  hao  mtoto  mmoja  amefariki  dunia.Amefahamisha  kuwa  wanatumia  taaluma  mbali  mbali  katika  kuhakikisha  wanapunguza  vifo  vya  mama  na watoto  hivyo  jamii  ni  lazima  kujenga  utamaduni  wa  kuvitumia  vituo  vya  afya  ili  kupata  uangalizi  wa  karibu  zaidi.

Kwa  upande  wao  wazazi  waliopo  katika  hospitali  hiyo  wamefurahia  huduma wanazozipata  katika  jengo  jipya  la  mnazimmoja   hivyo   wameiomba  serikali  kupitia  wizara  ya  afya  kuongeza   idadi  ya  vitanda  pamoja  na vifaa  vya  kujifungulia