WATOTO ELFU 30 WANATARAJIWA KUPEWA CHANJO

Zaidi ya watoto elfu 30 wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5 wa wilaya ya magharibi a na b wanatarajiwa kupewa chanjo za vitamin a na dawa za minyoo kwa kipindi cha mwezi mmoja ili kuwakinga na maradhi mbalimbali katika kipindi cha ukuaji wao.
Akizindua utowaji wa chanjo kwa watoto katika kituo cha afya magogoni, mkurugenzi wa manispaa magharibi ‘b’ amour ali, amesema watoto chini ya umri wa miaka mitano wamekuwa wakiatirika na kupata maradhi ikiwemo serua pepopunda, kuharisha na kupooza kutoka na ukosefu wa chanjo.
Amefahamisha kuwa chanjo zinaumuhimu mkubwa kwa watoto husaidia katika makuaji yao iwapo watapata lishe pamoja na matone ya vitamin a hali itakayosaidia kustawisha afya zao.
Daktari dhamana wilaya ya magharibi dr. Rahma maisara na mtaalamu wa afya na lishe kutoka unicef bi shemsa mselem, wamesema watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wamekua wakipoteza maisha kutokana na ukosefu wa chanjo kutokana na upungufu wa damu unaosababishwa na ukosefu wa vitamin
Nao wananchi waliopatiwa huduma hiyo wameunga mkono jitihada za serikali za kuwapatia chanjo watoto kwani zinasaidia kuwakinga na maradhi watoto wao jamabo ambalo hapo awali halikuwepo.