watoto mapinduzi cup

Katika kuhakikisha wadau wa soka wananchi wanaiunga mkono zbc kupitia mashindao ya zbc watoto mapinduzi cup mdau mkubwawa mchezo wa mpira wa miguu zanzibar na pia aliyewahi kuwa mshauri wa rais wa michezo wa awamu ya tano mh moh’d raza leo alifika office za zbc na kukabidhi zawadi za mashindano hayo Miongoni mwa zawadi hizo ni pamoja na kombe la mshindi ,fulana za kamati,medal za washindi za zahabu na fedha pamoja na kuongeza zawadi ya mfungaji bora,muamuzi bora na mchezaji bora pia kusema zawadi hizi katika kupamba mashindano zitakuwa na nembo za zbc Mkurugenzi wa wa shirika la utangazaji zanzibar aiman duwe alisema yeye na timu yake wamefarajika kwa kupata msaada huo kwa ajili ya kuwaendeleza vijama juu ya vipaji vyao Nae mwenye kiti wa kamati ya mashindano hayo akitoa neon la shukrani kwa mh raza alimshukuru na pia kumtaka aendelee kuiunga mkono zbc juu ya mambo ya maendeleo ya taifa kwa kuwaendeleza vijana wa kizanzibar na tanzania kwa ujumla