WATOTO WALIOKUWA HAWANA VYETI VYA KUZALIWA WAMETAKIWA KUANDIKISHWA SKULI

 

watoto waliokuwa hawana vyeti vya kuzaliwa wametakiwa kuandikishwa skuli umri unapofika na isiwe ni kikwazo cha kukosa haki hiyo ya msingi kitakachowarudisha nyuma katika maendeleo yao.

mkurugenzi idara ya elimu msingi na maandalizi bi safia ali  rijali ameeleza  hayo alipokuwa  akizungumza na masheha  wa  wilaya ya  kati na  kuwataka wafikishe  ujumbe  kwa walimu wakuu wa  skuli zote.

ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wazazi waliokosa nafasi ya kuandikishwa watoto wao kutokana na kukosa vyeti vya kuzaliwa.

nao masheha wa  wilaya  hiyo wamesema wanahitaji  kuongezewa  nguvu  katika   ujenzi  wa  madarasa  mapya  ili  kuweza  kumudu  wingi  wa  wanafunzi wapya katika kujiunga  na  masomo ya awali  na  msingi.

mkuu  wa  divisheni  ya madrasa   katika  idara  ya maandalizi na msingi amina salum khalfan amesisitiza  walimu  kusomesha kwa  nia  sio  kwa ajili  ya  kazi  tu ili  kurudisha  heshima na maadili  kwa  wanafunzi waweze  kufanikiwa.

mapema   bisafia  akizungumza  na  wazazi  na  walezi  katika  kijiji cha  kijibwemtu amewasisitiza  kuwaelimisha  watoto  wao  juu  ya  vitendo  vya  udhalilishaji ili waweze kujiepusha  navyo  kutokana  kushamiri  kwa  vitendo  hivyo  kila siku.