WATOTO WAPATAO 23 WAKIWEMO WAKIUME WAMERIPOTIWA KUFANYIWA VITENDO VYA UDHALILISHAJI

Watoto wapatao 23 wakiwemo wakiume wameripotiwa kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia katika kituo cha mkono kwa mkono cha kivunge, mkoa kaskazini unguja katika kipindi cha mwezi augosti hadi oktoba mwaka huu.
Takwimu hiyo imetolewa na afisa ustawi wa jamii mkoa huo nd. Mussa haji kessi wakati wa kongamano lililozungumzia vitendo vya udhalilishaji lililoandaliwa na jumuiya ya wanafunzi wa skuli za sekondari waliosoma marekani kupitia mradi wa yess (zanzibar yess allumni association) lililofanyika skuli ya elimu mbadala rahaleo.
Amesema takwimu hizo zinawahusu vijana waliopeleka taarifa zao katika kituo cha mkono kwa mokono, lakini wapo waliofanyiwa vitendo hivyo bila ya kutolewa taarifa kwenye kituo hicho na kesi zao kusuluhishwa mitaani.
Raisi wa jumuiya ya wanafunzi hao ndugu saidi ali ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kuihamasisha jamii kuwa na moyo wa kujitolea na kuelewa umuhimu wake katika maendeleo ya nchi na kusema imefanikiwa kusaidia masuala ya masomo kwa wanafunzi wa skuli mbali mbali unguja na pemba.
Katibu mkuu wa jumuiya hiyo ndugu msimu ali aliwashukuru wenyeji wao wanapokuwa marekani kwa mashirikiano mazuri wanayowapa jambo ambalo linawapa wepesi wa kutekeleza jukumu lao la kusoma.