WATU 11 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI NIGERIA

 

 

watu 11 wauawa katika shambulizi nigeria

watu wasiojulikana wamefanya shambulizi katika kanisa moja kaskazini mashariki mwa nigeria na kuwauwa watu 11 wameuawa huku wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya.

duru kutoka nchini humo zinasema watu waliokuwa na bunduki walifika katika jengo la kanisa hilo mapema jumapili asubuhi kwa kusudi la kumuua mtu mmoja ambaye hata hivyo hakuwepo na baadaye kufyatua risasi kuwalenga watu wengine waliokuwepo katika eneo hilo.

polisi wanasema tukio hilo linaweza kuhusishwa na biashara za madawa ya kulevya na kuwa huenda halijafanywa na kundi la boko haram ambalo mashambulizi yake yamesababisha kufungwa mamia ya makanisa kwenye ukanda huo katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.