WATU 12 WAMEMAKAMATWA WANAOTUHUMIWA NA UJAMBAZI.

 

Jeshi la polisi kanda maalumu ya dar-es-salaam limefanikiwa kukamata watu 12 wanaotuhumiwa kujihusisha na ujambazi.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi kanda maalumu ya dar-es-salaam kamishina simoni siro amesema majambazi hayo yalikamatwa kwa nyakati tofauti kufuatia oparesheni maalumu iliyofanywa na kikosi cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya jiji la dar-es-salaam.

Aidha kamishina  siro amesema kikosi maalumu cha kuzuia na kupambana na wizi wa magari cha jeshi la polisi kanda ya dar-es-salaam kimefanikiwa kuyakamata magari manne ambayo yaliibwa katika jiji la dar-es-salaam kipindi cha juma lililopita.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limemkamata mtuhumiwa idi bashiri (24) kwa kukutwa na bunduki moja aina ya mark 1v yenye risasi 3 ndani ya magazini akiwa ameihifadhi ndani ya begi lake, ambapo pia kufuatia oparesheni ya madawa ya kulevya inayoendelea jeshi hilo limewakamata  watuhumiwa 100 wa makosa ya kupatikana na madawa ya kulevya.