WATU 17 WAMEUAWA KUFUATIA MAPOROMOKO YA ARDHI NA MAFURIKO

Watu 17 wameuawa kufuatia maporomoko ya ardhi na mafuriko ambayo yamesababishwa na kimbunga cha kai-tak nchini ufilipino.
Polisi wamesema watu 30 hawajulikani waliko baada ya maporomoko hayo kutokea mji wa naval , kusini mashariki mwa mji wa manila.
Kimbunga kai-tak kilianza jumamosi mashariki mwa ufilipino na kimeendelea kuandamana na upepo mkali unaovuma kwa kasi ya kilomita 55 kwa saa.
Kulingana na watabiri wa hali ya anga, kimbunga hicho kinatarajiwa kusababisha mvua katika maeneo ya kati na magharibi mwa ufilipino.