WATU 17 WAMEUWAWA KATIKA MASHAMBULIO MAWILI YA MABOMU NIGERIA

Kiasi cha watu 17 wameuwawa katika mashambulio mawili ya mabomu yanayotuhumiwa kufanywa na kundi la boko haramu katika soko moja lililopo katika mji wa biu nchini nigeria.
Mji wa bau mekuwa ukikumbwa na mashambulizi ya wanamgambo wa boko haramu ambayo yamekuwa yakilenga maeneo yenye mikusanyiko na kusababisha vifo vya raia kadhaa.
Mashambulizi ya boko haramu katika maeneo mengi ya nigeria tokea kundi hilo lilipoanza uasi yamesabisha watu zaidi ya milioni moja na laki saba kuachwa bila ya makaazi na wengine zaidi ya elfu ishirini kuuwawa.