WATU 17 WAMEUWAWA KUFUATIA RISASI ZILIZOFYETULIWA

 

watu 17 wameuwawa kufuatia risasi zilizofyetuliwa na kijana wa miaka 19 katika skuli moja ya parkland katika jimbo la florida nchini marekani.

habari zinasema kuwa watu wengine 14 wanatibiwa hospitalini, na watatu kati yao hali yao ni mahtuti.

mshukiwa wa shambulizi hilo amekamatwa na polisi huku habari za polisi zikisema kijana huyo alifukuzwa katika skuli hiyo kwa makosa ya ukosefu wa nidhamu.

kwa mujibu wa seneta bill nelson, kiijana huyo alibonyeza kengele ya kutoa tahadhari iliyowafanya wanafunzi watoke nje.

wanafunzi wenzake wanamueleza kijana huyo kuwa mpweke lakini anapenda kuchezea silaha na visu.