WATU 17 WAMEUWAWA NA WENGINE WANNE WAMEJERUHIWA KWENYE SHAMBULIO LA KIGAIDI

Watu 17 wameuwawa na wengine wanne wamejeruhiwa kwenye shambulio la kigaidi lililotekelezwa katika mji mkuu wa burkina faso, ouagadougou.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema watu watatu waliokuwa na bunduki waliwafyatulia risasi wateja waliokuwa nje ya hoteli moja na mgahawa.
Waziri wa mawasiliano wa burkina faso remis dandjinou amesema haijabainika ni washambuliaji wangapi waliohusika katika tukio hilo.