WATU 19 WAUAWA KWENYE MLIPUKO MANCHESTER

 

Polisi nchini uingereza wanasema watu wasiopungua 19 wameuawa na wengine 59 kujeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea mwishoni mwa tamasha la muziki mjini manchester kaskazini magharibi mwa england.

Maafisa wawili wa marekani wamesema mshambuliaji wa kujitoa muhanga anashukiwa kuhusika na mlipuko huo.

Waziri mkuu wa uingereza theresa may amesema tukio hilo linachukuliwa kuwa la kigaidi ambapo pia  anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama kuanzia saa tatu asubuhi.