Watu 30 wauawa harusini Kaskazini mwa Baghdad

Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga wameuwa watu wasiopungua 30 waliokuwa wakisherehekea harusi katika kijiji kilichopo karibu na mji wa Tikrit, umbali wa km 170 Kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

Mashuhuda wamesema watu wengine 26 wamejeruhiwa katika shambulio hilo, lililotokea katika kijiji cha Hajaj.

Maafisa wa Usalama walilizingira eneo la shambulio hilo na kutangaza sheria ya hali ya hatari kwa kuhofia uwezekano wa kuwepo washambuliaji wengine.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika, lakini mashambulio kama hayo yamekuwa yakifanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, kulipa kisasi kwa mashambulizi dhidi yao yanayofanywa na vikosi vya serikali katika mji wa Mosul.