WATU 33 WAUAWA SYRIA

Zaidi ya watu 30 wameuawa nchini syria katika shambulizi la anga lilofanywa na majeshi ya muungano yanayoongozwa na marekani katika shule inayotumika kama kituo cha watu wasio na makaazi karibu na mji unaodhibitiwa na kundi la dola la kiislamu is.
Shirika la haki za binaadamu nchini syria lenye makao yake london, uingereza limesema shambulizi hilo kwenye mji wa al-mansoura, kaskazini mwa jimbo la raqa lilifanyika mapema wiki hii.
Mapema mwezi huu jeshi la muungano limesema mashambulizi nchini syria na iraq yaliwaua bila kukusudia kiasi ya raia 220, ingawa waangalizi wanasema idadi ya raia waliouawa ni zaidi ya hiyo.