WATU 80 WAMEUWAWA BAADA YA BOMU LILILOTEGWA KATIKA GARI

Watu wapatao 80 wameuwawa na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa baada ya bomu lililotegwa katika gari kuripuka katika mjini mkuu wa afghanistan, kabul.
Polisi imethibitisha kwamba mlipuko huo ulitokea karibu na ubalozi wa ujerumani, katika eneo ambapo kunapatikana ofisi mbalimbali na majengo muhimu ya serikali.
Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo. Huku kukidaiwa kuwa hali ya usalama bado ni mbaya nchini humo ambako majeshi yake yanakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wapiganaji wa itikadi kali.