WATU WA ULEMAVU ZNZ WANASHERIA KUJIFUNZA LUGHA ZA ALAMA ILI KUWASAIDIA MAHAKAMANI

 

idara ya watu wa ulemavu zanzibar imesema inaendelea na juhudi za kuhamasisha wanasheria kujifunza lugha ya alama ili kusimamia kesi za watu wenye uleamavu mahakamani.

mkurugenzi idara hiyo abeda rashid abdalla lengo la serikali ni kuhakikisha watu hao wanapata haki zao ikwemo za kisheria.

akizungumza katika mkutano wa mkuu wa chama cha viziwi zanzibar chaviza huku ameiomba pia jamii kujifunza  lugha hizo za alama ili kundi hilo lipate taarifa kwa wakati.

nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo wameelezea namana wanavyokabiliana na matatizo mbalimbali hasa wanapowasiliana na jamii na taasisi mbalimbali.

mwenyekiti barza la watu wenye ulemavu haidar madowea amesema jumuiya hiyo inanafasio katika kuendeleza shughuli zake iwapo itazingatia katiba.