WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI WEZI WAMEWAIBA NA KUWACHINJA MBUZI 13

Watu wanaosadikiwa kuwa ni wezi wamewaiba na

kuwachinja  Mbuzi 13 wa wafugaji wawili tofauti

katika kijiji cha  Fuoni Birikau

tukio hilo limetokea usiku wa jana majira ya saa kumi za usiku wakati wafugaji wa mbuzi hao wakiwa wamelala.

mmiliki mmoja wa mbuzi hao ambae ameibiwa mbuzi tisa ndugu Makame Salum ameliomba Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi ili kuwasaidia wafugaji ambao lengo lao ni kujiondoa katika umasikini.

ameelezea kuhuzunishwa na tukio hilo lililomsabababishia kupata hasara ya shilingi laki sita.

mfugaji mwengine wa mbuzi aliyepatwa na mkasa huo ni ndugu ali masoud aliyefungiwa mlanvgo wa nyumba yake kwa nje na kisha kuibiwa Mbuzi wanne.

kamanda wa polisi mkoa  Mjini Magharibi Hassan Nassir hakupatikana kuzungumzia tukio hilo .