WATU WANNE WAMEJERUHIWA NA NYUMBA 133 ZIMEHARIBIKA

 

 

Watu wanne wamejeruhiwa na nyumba 133 zimeharibika kati ya hizo nyumba 60 zimeizuliwa mapaa kwa upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa ilionyesha huko tumbatu kichangani majira ya saa saba mchana siku ya jumamosi.wakizungumza na zbc wahathirika wa upepo huo wamesema walisikia kishindo kikubwa ndipo walipotoka na kuangalia na kukuta upepo unabomoa nyumba katika maeneo ya tumbatu kichangani hivyo wameiomba serikali na viongozi wa siasa kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu ili waweze kuishi kama kawaida.

Nae katibu tawala wa wilaya hiyo ndu: mohamed omari hamadi alifika kuwapapole waathirika hao na kuwataka kuwa wastamilivu kwa kipindi hiki kwani serikali ipo pamoja nao watashirikiana katika kuirejeshea hali yao ya  kawaida.