WATU WAPATAO WATATU WAMEUAWA BAADA YA LORI LILILOKUWA LIMEBEBA GESI ASILIA KUSHIKA MOTO

Watu wapatao watatu wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebeba gesi asilia kushika moto katika mji mkuu wa ghana, accra, na kusababisha milipuko katika vituo viwili vya kuuzia mafuta.
Msemaji mkuu wa huduma ya kuzima moto taifa, amesema watu wawili wamefariki dunia katika eneo la tukio jana usiku na mmoja amekufa hospitali.
Naibu waziri wa habari, kojo nkrumah, amesema serikali imetumia magari 12 ya kuzima moto na maafisa wa polisi 200 wa kusimamia na kudhibiti msongamano katika eneo hilo la legon.
Tukio hilo la hivi karibuni limezusha hasira miongoni mwa wananchi wa ghana katika mitandao ya kijamii, kuhusu usalama wa vituo va kujazia mafuta ambavyo vingi vipo karibu na skuli, hospitali na maeneo ya biashara.
Mwezi juni mwaka 2015 kituo kingine cha kuuzia mafuta ya petroli kililipuka na kusababisha vifo vya watu wapatao 150.