WATU WAWILI WAUWAWA KENYA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI KUTANGAZWA

Watu wawili wameuwawa katika mji wa kisumu magharibi mwa kenya baada ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani raila odinga kufanya vurugu kupinga matokeo ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, watu hao waliuwawa kwa kupigwa risasi katika vurugu hizo ambazo zilianza muda mfupi baada ya rais uhuru kenyatta kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliomalizika nchini kenya.
Wafuasi hao wamekuwa wakipambana na polisi katika mitaa mbalimbali ambayo imekuwa na wafuasi wengi wanaomuunga mkono raila odinga katika jiji la nairobi.