WATU WENYE ULEMAVU KATIKA MKOA HUO KUANZISHA JUMUIYA YA PAMOJA

 

 

Mkuu wa mkoa   wa kusini unguja mhe hassan khatib hassan amewashauri watu  wenye ulemavu katika  mkoa huo kuanzisha jumuiya ya pamoja  itakayowawezesha kurahisisha upatikanaji wa mahitaji yao.

Wito huo ametoa katika hafla fupi ya kuwakabidhi vifaa vya visaidizi watu wenye ulemavu wa mkoa huo ikiwa ni msaada kutoka serikali ya  kuwait kupitia ofisi ya makamo wa pili wa rais .

Amesema uanzishwaji wa jumuiya ya pamoja kwa watu wenye ulemavu ndani ya mkoa huo ni muhimu kwani itawawezesha kupata fursa  mbali mbali zikwemo  elimu, mikopo, ruzuku na misaada  kutoka kwa taasisi na wahisani  ndani na nje ya nchi.

Aidha amewasisitiza wazazi na walezi wanaoishi na watoto wenye ulemavu kuondokana na tabia ya kuwaficha watoto wa aina hiyo na badala yake kuwapatia elimu kwa ajili ya kuwajengea mustakbali mzuri wa maisha yao ya baadae .

Nae afisa wa watu wenye ulemavu mkoani humo ndugu mabula machanila nalimi amesema idara ya watu wenye ulemavu zanzibar itaendelea kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu ili kuona kuhakikisha wanapata haki sawa kama watu wengine.

Nao watu wenye ulemavu wakipokea visaidizi hivyo wameishukuru serikali kwa jitihada zake za kuwathamini na kusema kuwa  msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya shughuli zao kwa urahisi.

Wakati huo huo mkuu  wa mkoa  kusini unguja kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya  mkoa walifanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mahafali ya chuo kikuu cha taifa suza tunguu na kuelezea kuridhishwa kwake na hatua ya ujenzi huo ulipofikia.