WATU WENYE ULEMAVU WANAWEZA KUJIAJIRI WENYEWE NA KUWEZA KUJIPATIA KIPATO

 

Ulemavu imeelezwa kuwa sio sababu ya kumfanya mtu kuwa omba omba kwani anaweza kufanya kazi mbali mbali za kumuwezesha kujipatia kipato kwa ajili ya kujikimu kimaisha.Ushirika wa watu wenye ulemavu znz ,  zanzibar  dis ability vegetable  katika kuhakikisha unapambana na umasikiini na kujipatia kipato ili kuachana na hali hiyo  kwa makusudi wameamua kuanzisha mradi wa kilimo cha mboga mboga na mazao mengine ya kibiashara huko dole wilaya ya magharibi a .

Naibu mwenyekiti wa ushirika huo ndugu mohammed khamis amesema watu wenye ulemavu wanaweza  kujiajiri wenyewe na pia  kushirikiana na watu wengine  katika jamii .Ramadhan andrea  na jomo shaaban  ni baba wa familia licha ya kuwa ni walemavu wa viungo lakini  wanajishughulisha na kazi mbambali ikiwemo kilimo kutembeza watalii lengo likiwa ni kujipatia kipato na kuondokana na utegemezi.

Nae mfuatiliaji wa miradi katika ushirika huo ndugu muhamadi abdalla akatoa  wito kwa watu wenye ulemavuUshirika wa dis ability vigitables umewaomba wafadhili na taasisi kujitokeza kuwasaidia ili kuuwezesha ushirika huo kutimiza malengo yake ushirika ambao una   wanachama 10 ikiwemo wanawake 2 na wanaume 8 lengo kuu la ushirika huo ni kuondosha matatizo kwa watu wenye ulemavu ili kujiepusha na  omba omba na kuwa tegemezi bila ya kufanyakazi.