WATU WENYE UWEZO KUENDELEA KUSAIDIA HUDUMA MBALI MBALI

Kada wa chama cha mapinduzi ndugu yasmin aloo amewataka watu wenye uwezo kuendelea kusaidia huduma mbali mbali za kijamii ili kustawisha maisha  ya wananchi masikini.

Mwanasiasa huyo ametoa wito huo wakati akikabidi dawa katika hospitali ya wagonjwa wa akili iliopo kidongo chekundu mjini zanzibar na kusema wananchi wengi ni maskini wanaohitaji kupatiwa misaada.

Alisema pamoja na serikali kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika sekta ya afya lakini wananchi wanapaswa kuiunga mkono kwa misada kama hivyo hasa ukizingatia ianakabiliwa n a majukumu mengi kuyatekeleza.

Hospitali hiyo ndugu khamis othman amesema dawa hizo za kutibu maradhi ya kifafa zitawasaidia sana na kumpongeza kiongozi huyo kwa kuwa na utaratibu wa kuisaidia hospitali ya kidongo chekundu mara kwa mara.