WATUMISHI WA WIZARA ELIMU KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO YA UTUMISHI WA UMMA

 

Mkurugenzi uendeshaji na utumishi katika Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Nd. Omar Ali amewataka watumishi wa wizara hiyo kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utumishi ili kutekeleza majukumu yao bila ya vikwazo.

Akifungua mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa wizara hiyo katika ukumbi wa skuli ya haile salassie amesema iwapo watumishi hao watazingatia misingi hiyo wataweza kusimamia haki na wajibu wao kikamilifu jambo ambalo litaleta tija katika utumishi wao.

Amaesema iwapo watumishi wa umma watazingatia dhana za ukuu wa sheria, usawa  na matumizi mazuri ya madaraka wataweza kufanya kazi kwa uweledi, ustadi na kuepukana na migogoro isiyo ya lazima.

Mapema akimkaribisha mkurugenzi huyo, mkurugenzi wa chuo cha utawala wa umma ipa dr, mwinyi talib, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya hitaji la kisheria hivyo washiriki wanapaswa kuyazingatia ili kuweza kuyatumia kikamilifu katika majukumu yao ya kila siku.

Mada mbili ziliwasilishwa na wakufunzi mwalim abdalla juma na hassan juma  kutoka chuo cha utawala wa umma ipa ambapo wamewasisitiza watumishi haokutofanya makosa ya kiutumishi yakiwemo utoro, uzembe na ubadhirifu wa mali za umma.

Jumla ya watumishi 1195 kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali wanatarajiwa kupatiwa mafunzo hayo kwa Unguja na Pemba.