WAUGUZI NA MADAKITARI KUTUMIA LUNGA NZURI PALE WANAPOKUWA WAKITEKELAZA MAJUKUMU YAO

Wauguzi na madakitari watakiwa kutumia lunga nzuri pale wanapokuwa wakitekelaza majukumu yao na kuzifuata sheria na taratibu za kazi zinavyo waelekeza ili kupunguza malalamiko kwa jamii wakati wanapokuwa katika sehemu zao za kazi
Mkurugenzi utawala wa hospitali kuu ya mnazi mmoja dr aboubakar khamis ametowa kauli hiyo wakati akuzungumza na wauguzi wa hospitali ya muembe ladu katika hafla ya kuwaaga wastaafu baada ya kutumikia taifa kwa kipindi cha muda mrefu
Amesema kazi yoyote inahitaji uvumilivu mkubwa na moyo wa kujitolea kutokana na pale linapotokezea tatizo kuwa na uvumilivu na upendo katika kufanikisha mahitaji ya wananchi na jamii inayowazunguka
wafanyakazi wanawajibu wa kutafakari kwa kile wanachokifanya na pia wawe tayari kujifunza ili waweze kujijengea sifa kwao na taifa kwa ujumla
Baadhi ya waudguzi wa hospitali ya muembe ladu wamewataka wafanyakazi kujituma zaidi na kuachana kufanya kazi kwa mazewea huku wakiahidi kuboresha huduma za mama wayawazito ili kupuguza vifo vitoka navyo na hali hiyo
wakitoa nasaha zao wastaafu hao wamesema wako tayari kuitumikia jamii kwa hali na mali huku wakiwataka wezao kuacha tofauti zao na kufanya kazi kwa kujitolea bila ya kuweka maslahi mbele