WAUGUZI NA WAKUNGA KUHAKIKISHA WANATOA HUDUMA NZURI KWA WAGONJWA

Naibu spika wa baraza la wawalishi mh mgeni hassan juma amewaagiza waunguzi na wakunga kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wagonjwa bila kufanya ubaguzi wowote wakati wanapotoa matibabu.
Akifungua kongamano kwa wauguzi na wakunga juu ya kushuka kwa maadili katika kazi zao amesema hatua hiyo itasaidia kwa wagonjwa hao kuwa na imani na wauguzi juu ya huduma wanazopatiwa.
Amesema kuna baadhi ya wauguzi hawafanyi kazi ipasavyo na kusababisha kuwepo kwa malalamiko mengi kwa wananchi hali ambayo inarejesha nyuma juhudi ya serikali katika kuwapatia huduma za afya kwa wananchi wake
Nae waziri wa afya mh mohmoud thabit kombo amewataka wauguzi kuwa na lugha nzuri wanapowahudumia wagonjwa ili kuimarisha utoaji wa huduma zao katika hospitali mbalimbali.
Kwa upande wao waguzi wamesema wakati umefika kwa wagonjwa kutoa taarifa katika uongozi pale wanapotolewa lugha chafu ili kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watendaji wasiokuwa waadilifu Katika kongamano hilo mada mbali mbali ziliwakilishwa na viongozi wa dini juu ya maadili ya waunguzi na faida zake katika dini.