WAUGUZI WA VITUO VYA AFYA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUFUATA MAADILI YA KAZI YAO

 

 

Waziri wa nchi ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mhe, issa haji gavu amewataka wauguzi  wa vituo vya afya kutekeleza majukumu yao  kwa kufuata  maadili ya kazi hiyo na misingi ya sheria .Nasaha  hizo amezitowa wakati akizindua kituo cha huduma ya afya kwa mama na mtoto cha umbuji ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya kuadhimisha miaka 54 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar.

Amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar itaendelea kutekeleza  azma yake ya kuwapatia wananchi huduma bora za afya na nyingine  kwa kuwajengea vituo vya afya karibu na maeneo yao ili kuweza kupata huduma  hiyo  kwa urahisi.Naibu katibu mkuu wizara ya afya bi halima maulid amesema kituo hicho kimejengwa chini ya ufadhili wa shirika la urio na serikali ya mapinduzi ya zanzibar na kuharimu zaidi  ya shilingi milioni mia mbili.

Akisoma risala kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha umbuji nd. Haji shauri wameishukuru wizara ya afya kwa kuweza kuwatatulia tatizo la kituo cha afya ambacho kilikuwa ni tatizo  kubwa.Mapema akimkaribisha mgeni rasmi waziri wa afya mh. Mahmoud thabit kombo amesema zanzibar ni nchi ya tatu ulimwenguni  katika utowaji wa huduma bora za afya, na kuahidi serikali itaendeleza mafanikio hayo