WAUMINI WA DINI YA KIISALAMU WAMESHAURIWA KUISOMA NA KUIFAHAMU QUR-ANI MAANA YAKE

Waumini wa dini ya kiisalamu wameshauriwa kuisoma na kuifahamu qur-ani maana yake ili kufikia lengo aliloamrisha mwenyezi mungu juu ya kitabu hicho kwa waumini hao.
Utalii utamaduni na michezo khatibu juma mjaja amesema waisalamu wasiichukulie qur-ani kama kitabu cha kutupwa na wajenge utamaduni wa kuisoma kwa kutekeleza yaliyoandikwa kwani haikusahau kitu.
Mdhamini mjaja ametowa ushauri huo skuli ya sekondari shamiani kwenye mashindani ya tah-fidhi qur-ani yaliyowashirikisha wanafunzi wa skuli ya madungu na shamiani.
Akielezea lengo la kuanzisha mashindani hayo kwa wanafunzi wa skuli hizo mwalimu mkuu wa skuli ya madungu mohamed shamte amesema ni kuwajenga vijana hao katika elimu ya dunia na akhera sambamba na kuwa waadilifu katika maisha yao ya baadae.
Huu ni mwaka wa pili kwa skuli ya shamiani na madungu kuandaa mashindani ya qur-ani kwa wanafunzi wao kwa juzuu ya tatu, yatano, yakumi na thalathini.