WAUMINI WA DINI YA KIISLAM WAMETAKIWA KUSHIKAMANA KATIKA HARAKATI ZA KUENDELEZA UISLAMU

 

 

Mwakilishi wa jimbo la uzini mhe, mohammed amewataka waumini wa dini ya kiislam kushikamana katika harakati za kuendeleza uislamu nchini.Aidha ametaka pia kuacha tabia ya kubaguana  kutokana madhehebu ya kila kundi na kusema jambo hilo halisaidii kukuza uislamuMhe, raza ameyasema hayo wakati wa hafla ya ya chakula cha mchana alichowandalia wanafunzi wa chuo kikuu cha zanzibar (suza) walioshiriki katika mashindano ya kuhifadhi qur an huko vuga.

Amesema asilimia kubwa ya wananchi wa zanzibar ni waislamu hivyo jukumu la kuhakikisha uislamu hauporomoki ni la kila muislamu visiwa hapa.Wakitoa shukran wanafunzi hao wamesema wamefarajika na uungwana wa mhe, mohhamed raza na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano wa mwema wa kiongozi huyo .Mbali ya chakula hicho pia mh.raza aliwakabidhi zawadi mbali mbali wanafunzi hao zikiwemo simu za mkononi.