WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAMETAHADHARISHWA KUTOA MAAMUZI YA USULUHISHI

Waumini wa dini ya kiislamu wametahadharishwa kutoa maamuzi ya usuluhishi wa masuala ya dini yao bila ya kuwa na elimu ya uelewa wa mambo ya dini ambayo msingi wake umejengwa na wanazuoni waliopita.
Akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu katika kongamano la wajibu wa wanazuoni na walinganiaji dini katika kuelekeza kuufahamisha umma uhakika wa uislamu, mkuu wa chuo cha darwil mustafa kutoka yemen,sheikh omar bin hafidh amesema sifa ya muumini wa kweli ni kuwa na tabia njema na kuepuka maamuzi yasio sahihi.
Amesema kuwa historia inaeleza kuwa nchi za afrika mashariki zilijijengea sifa ya kuwa na wanazuoni walioheshimika kutokana na kuwa na elimu kubwa ya dini ambayo iliwawezesha kutoa maamuzi ya kidini bila ya kutokezea kutofahamiana kwa waumini kwa wakati huo.
wakitoa mada katika kongamano hilo sheikh khamis abdulhamid na abubakar baalawiy wamekumbusha juu ya umuhimu wa kuwaunganisha waislamu, kusameheana huku wakihimiza namna ya kuishi kwa wema na majirani.
msimamizi wa kongamano hilo sheikh samir zulfikar amesema kupitia kongamano hilo waisalamu watafaidika kupata fursa ya kuonyesha umoja kupitia dini yao pamoja na kujua majukumu ya uislamu.
Kongamano hilo la siku moja limewakutanisha masheikh kutoka nchi ya yemen, saudi arabia, afrika kusini, kenya, tanzania bara na wenyeji zanzibar.