WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAMETAKIWA KUJENGA TABIA YA KUWEKA FEDHA

Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kujenga tabia ya kuweka Fedha zao kidogo kidogo ili waweze kwenda kushiriki katika ibada ya Hija nchi Saud Arabi.

hayo yamesemwa katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu julius nyerere jijiini Dar es salaam na baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu  waliozungumza na ZBC ambapo wamesema ibada ya hija ni nguzo muhimu kwa  Muislamu hivyo wametakiwa kuweka akiba ili aweze kwenda kutekeleza ibada hiyo.

Dkt Muhsin Masoud ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Amana ambapo amesema kwa kutambua umuhimu wa idaba ya hija benki hiyo imeanzisha akaunti maalumu itakayomwezesha mtu kuweka Fedha zake kidogo kidogo ili aweze kwenda kutekeleza ibada hiyo.