WAVUVI 53 WALIOPATA AJALI TUMBATU WAMEPATIKANA.

 

Mamlaka ya usafiri baharini zanzibar (zma) imesema wavuvi 53 waliopata ajali na boti ya uvuvi maeneo ya mwamba said kilomita 12 kutoka kisiwa cha tumbatu wamepatikana.

Wavuvi hao waliripotiwa kupotea baharini baada ya chombo chao kinachoitwa  advantage kuzama walianza katafutwa kufuatia  mwenzo mmoja kuokolewa na meli ya sealink iliyokuwa ikitokea pemba.

Kwa mujibu wa baadhi ya  taarifa zilizotolewa na watu mbalimbali wakiwemo wavuvvi wenyewe zinaeleza kuwa wavuvi 40 waliogolea hadi kisiwa cha tumbatu na wengine wakaokolewa kwa nyakati tofauti watatu kati yao walipelekwa hospitali ya kivunge baada ya kuonekana hali zao haziridhishi.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa zma, bi. Sheikha ahmed mohd amesema ajali hiyo imesababishwa na kuchafuka kwa bahari kufuatia hali mbaya ya hewa

Sheikh amewashauri watumiaji wa bahari wanaotumia vyombo vidogo kuzingatia taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa na kufuata taratibu za usalama baharini.