WAVUVI NA MAMALISHE WALIO NA VIBANDA KUTEKELEZA AGIZO LA KUVIONDOA VIBANDA HIVYO

Mkuu wa wilaya magharibi ‘b’ kapteni silima haji, amewataka wavuvi na mamalishe walio na vibanda katika soko la mazizini kutekeleza agizo la kuviondoa vibanda hivyo ili kutoa nafasi ya kufanyika usafi wa mazingira katika eneo hilo.
Kapten silima amesema vibanda hivyo vipo kinyume na utaratibu na havina muonekano mzuri katika suala la usafi wa mazingira na kwamba uwepo wake unapelekea athari nyingi ikiwemo uchafuzi wa mazingira.
Akishiriki katika zoezi la usafi uliofanyika katika katika soko la samaki mazizini silima ameitaka manispaa magharibi b kulisimamia zoezi la kuhakikisha vibanda hivyo vinaondoka kwa muda waliotakiwa kwani wamiliki wa vibanda hivyo walishapewa muda wa kuviondoa lakini bado wanaendelea kukaidi agizo hilo.
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais mh; moh’d aboud moh’d amesema kufanyika kwa usafi katika maeneo ya soko la samaki mazizini kumetokana na kuibuka kwa vitendo viovu ambavyo vikiachiwa vinavyopelekea usumbufu kwa watumiaji wa eneo hilo.
Kwa upande wake, diwani wa wadi ya mbweni maabadi ali maulid, na wananchi wa maeneo hayo wamesema wilaya yao inakabiliwa na tatizo la uchafuzi wa mazingira, hivyo wamewaomba wananchi kujenga utamaduni wa kudumisha usafi ili kujipusha na mripuko wa maradhi.