WAVUVI WA TUMBATU WAMEKUBALI KUWEKA ENEO KUZALISHA MAZAO YA BAHARINI

 

Wavuvi  wanaoendesha   shuhuli  zao  katika   bahariYa  tumbatu  na maeneo  ya  jirani  wamekubali

Kuweka   eneo  maalum  la  hifadhi ya bahari  ili Kuzalisha mazao  ya  baharini.Makubaliano hayo yamefikiwa kufuatia bahari hiyo ya tumbatu kupoteza hadhi yake ya kuwa na samaki wengi iliyosabishwa na uharibifu wa mazingira.

Jumuiya  ya  maendeleo  ya  tumbatu  jongowe  ikishirikiana  na  mtandao  wa  mwambao  tanzania   pamoja  na  viongozi  mbali mbali   wametoa  elimu  ya  uhifadhi   wa  bahari  na  faida  zake  na  kufikia  makubaliano hayo.

wakitoa  maoni  yao  katika   semina  iliyoandaliwa na jumuiya  hizo  watumiaji wa bahari ya tumbatu wameshauri  mambo  mbali mbali  yatayosaidia  kufikia  lengo  lililokusudiwa.

Semina   hiyo  iliyofanyika   chuo cha mafunzo ya amali  mkokotoni  imeendeshwa  na mkufunzi  dr.  Mohamed  makame kutoka   ofisi  ya  raisi  tawala  za  mikoa,serikali  za mitaa,na  idara  maalum  za  smz,na  ndugu  ali  abdul-rahim  kutoka  mtandao  wa  mwambao  tanzania.