WAVUVI WANAOJISHUGHULISHA NA UVUVI HARAMU PAMOJA NA KUTOKUWA NA LESENI

Idara ya maendeleo ya uvuvi imefanikiwa kuwakamata wavuvi wanaojishughulisha na uvuvi haramu pamoja na kutokuwa na leseni za uvuvi katika ukanda wa ghuba ya chwaka.
Akizungumza wakati wa doria mkurugenzi wa idara hiyo mussa aboud jumbe amesema kati ya wavuvi hao waliokamatwa wamo wanaotumia uvuvi wa kuchupa ambao hutumia vioo, viatu, mikuki na wengine wanatumia nyavu za kukokota.
Amefahamisha kuwa kwa mujibu wa sheria uvuvi wa kutumia vioo au viatu na nyavu za kukokota hauruhusiwi kutokana na kuharibu matumbawe na mazalia ya samaki na kusisitiza kuwa idara haitosita kumchukia hatua za kisheria mtu yoyote atakaekamatwa kwa kufanya vitendo hivyo.
Nd. Jumbe amesema katika ghuba hiyo samaki wengi wamepotea kutokana na uvuvi haramu hivyo ametaka wavuvi kuacha tabia hiyo kwa faida yao na vizazi vijavyo.
Idara ya maendeleo ya uvuvi imefanya doria hiyo katika bahari ya marumbi, chwaka, uroa, michamvi, pongwe na kiwengwa na kufanikiwa kukamata vifaa mbali mbali vinavyotumika katika uvuvi haramu.