WAWAKILISHI WAMESHAURI BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI KUWA MAKINI KATIKA BIDHAA ZINAZOTOKA NJE

wajumbe wa baraza la wawakilishi wameshauri bodi ya chakula, dawa na vipodozi (zfdb) kuwa makini katika bidhaa zinazotoka nje ya nchi hasa mchele, mafuta na vitoweo , ili kulinda afya na usalama kwa wananchi.
wakichangia mada katika semina ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wamesema kuibuka ongezeko la uingizwaji wa bidhaa zisizo na viwango hali ambayo inayowafanya watumiaji wa bidhaa hiz kuwa na hofu juu ya afya zao.
wameeleza kuwa ipo haja ya zfdb kutoa elimu kwa jamii juu ya kutathmini bidhaa wanazonunua kabla ya kuzitumia pamoja na kuwaelimisha wafanya biashara hasa katika masoko ya nyama na kuweka mazingira ya ubora katika maeneo ya biashara zao ili kuepusha maradhi ambayo yanayoweza kutokea nchini.
akiwasilisha mada ya bodi ya chakula dawa na vipodozi, dr burhani othman amesema licha ya mafanikio waliyoyapata lakini wanakabiliwa na changamoto ikiwemo kughushiwa kwa bidhaa na nyaraka (document) kunakofanywa na wafanya bishara wasiokuwa waaminifu hali ambayo inawafanya kurejesha nyuma kazi zao.
nae naibu wa afya kwaniaba ya waziri wa afya mh’ mahmoud thabit kombo mh’ harusi said amesema lengo na madhumuni ya semina hiyo ni kuiyelewa na kuifahamu ili itakapofika kuichangia katika barazaza la wawakilishi waweze kuchangia kwa umakini pamoja na kuiwezesha jumuiya ya zfdb kuweza kushiriki kikamilifu katika mashirikiano y jumuiya ya afrika mashariki na umoja wa afrika.